Wanafunzi Chuo cha Ustawi wa Jamii wakusanya vikombe SHIMIVUTA Tabora
06 January 2026
Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii Dkt. Joyce Nyoni amepokea ujumbe wa wanafunzi walioshiriki mashindano ya #Shimivuta yaliyofanyika mkoani Tabora kuanzia tarehe 11 hadi 23 Desemba 2025. Katika michuano hiyo timu za wanafunzi wa #ISW zimetwaa vikombe, medali na vyeti vya ushindi kama ifuatavyo; medali ya mshindi wa pili mbio za mita 400 wanawake, kombe la mshindi wa tatu karata, kombe la mshindi wa kwanza mbio za magunia na cheti cha timu yenye nidhamu bora mshindi wa pili. "Ni heshima kubwa kwa chuo kwa ushindi huu mlioupata, ushindi huu uwe mfano na kipimo cha juhudi za kufanya vyema zaidi mashindano yajayo," alisema Dkt. Joyce. Kwa mujibu wa mkuu wa chuo, ameeleza kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kuwafanya wanafunzi kuwa imara na shupavu. Aidha, aliwahimiza kuendelea na mazoezi kwa kuwa michezo huchochea ufaulu katika masomo yenu, huongeza mahusiano mema katika ya vyuo na wanafunzi wenzenu kutoka vyuo mbali mbali. Naye, Selemani Mwenda Kiongozi wa Michezo kutoka Serikali ya Wanafunzi (ISWOSO), amemuahidi Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kuwa wataongeza ushawishi kwa wanafunzi wengi kushiriki michezo ili kuibua vipaji ambavyo baadaye huzaa ajira na kipato kwa kila mmoja ambacho huchangia maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla