Chuo cha Ustawi wa Jamii

CHETI CHA SHUKRANI

Serikali, kupitia Wizara ya Fedha, imeitunuku Chuo cha Ustawi wa Jamii Cheti cha Shukrani kwa kutambua mchango unaotolewa na chuo katika kutoa huduma kwa Jamii. Huduma hizo ni ushauri nasihi pindi maafa mbalimbali yanapotokea nchini, ushauri kwa vijana na familia na kuchangia katika kuimarisha huduma za ustawi wa jamii kwa wananchi wa makundi yote, hasa wenye uhitaji zaidi.

WANAFUNZI WAELIMISHA RIKA (Peer Educators) WAFUZU MAFUNZO ISW

Mkuu wa chuo Dkt. Joyce Nyoni amewatunuku vyeti Waelimisha rika "peer educators" ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii walikuwa sehemu ya kupata mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Unesco Tanzania kwa Kushirikiana na Chuo cha Ustawi wa Jamii chini ya mradi wa O3 Plus. Hafla hiyo ya kuhitimisha Mafunzo ya Waelimisha rika katika masuala ya Jinsia, Kuzuia ukatili wa kijinsia na UKIMWI, imefanyika tarehe 04 Februari, 2025 katika kampasi ya Dar es Salaam ambapo wahitimu 20 wamefuzu mafunzo hayo. Kabla ya kutunuku vyeti Dkt. Joyce amewapongeza wanafunzi hao kwa kutenga muda wao kujifunza masuala ya Kuzuia Ukatili wa kijinsia na UKIMWI pia amewasisitiza wahitimu hao wakawasaidie wanafunzi wenzao hususan wanafunzi wa ngazi ya Cheti kuelimishwa juu ya masuala ya Kuzuia Ukatili wa Kijinsia na UKIMWI. Aidha kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa 03 Plus kwa Dar es Salaam, Bi Numbilya Kiseko amewasisitiza wahitimu hao wakawe madaraja na chachu ya kuwapa wanafunzi taarifa sahihi na kuwaelimisha wanafunzi wenzao juu ya masuala ya kuzuia ukatili wa kijinsia na UKIMWI. Mafunzo haya yamewajengea uwezo na kuwapa maarifa wahitimu ambao watakuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha wanafunzi juu ya masuala ya mahusiano, kuzuia ukatili ya Kijinsia na UKIMWI.

MKUTANO WA MAPITIO YA MITAALA

Chuo cha Ustawi wa Jamii chakutanisha wawakilishi wa mashirika ya kitaifa na kimataifa, pamoja na wahadhiri na wanafunzi wa Chuo cha Ustawi Wa Jamii tarehe 24, Januari 2025 Katika kampasi ya Dar es Salaam kujadili mapitio ya mitaala. Akizungumza katika mkutano huo Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Sotco Komba amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za elimu na wadau wa maendeleo ya jamii ili kuhakikisha mitaala hiyo inakidhi mahitaji ya sasa ya kijamii na soko la ajira. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na uboreshaji wa mitaala ili iendane na mabadiliko ya kijamii na teknolojia, kuimarisha mafunzo kwa vitendo kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali, na kukuza matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ufundishaji na kufanya tafiti..

TAMASHA LA KIMATAIFA LA MAENDELEO YA FILAMU NA SANAA

Chuo cha Ustawi wa Jamii chashiriki Tamasha la kimataifa la Maendeleo ya Filamu na Sanaa lililofanyika katika viwanja vya Posta, Kijitonyama Dar es Salaam kuanzia tarehe 11 Desemba na kumalizika tarehe 15 Desemba . Aidha wanafunzi wa chuo ustawi wa jamii walipata nafasi ya kushiriki katika mdahalo kuhusu Jinsia na Sanaa, mdahalo ambao uliitwa "Binti Longa Gender" na Kubadilishana mawazo na wasanii na wawezeshaji katika mdahalo huo.

Kumbi za Mihadhara Kuongezwa ISW

Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni, amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa mapya unaoendelea katika Kampasi ya Dar es Salaam, ambapo hadi sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 16 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo Mwanzoni mwa Mwaka 2025. Mradi huu unalenga kuboresha miundombinu ya kujifunzia katika kampasi ya Dar es Salaam.

Site Visitors
Today
463
Yesterday
951
This Week
6,295
This Month
23,413
All days
580,648
Online
2
Video