Mkutano wa 5 wa wadau na wanafunzi wa uanagenzi wajadili mwelekeo na mafanikio ya programu ya uanagenzi
06 December 2025
Mkutano wa 5 wa Wadau na Wanafunzi wa Uanagenzi kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii umefanyika katika Kampasi ya Dar es salaam, ukiwakutanisha wamiliki wa Taasisi mbalimbali pamoja na Wanafunzi wanaotarajia kuanza mafunzo ya vitendo kupitia programu ya uanagenzi. Mkutano huu umefanyika kuanzia tarehe 2 – 5 Desemba, 2025. Kwa mwaka huu, programu ya uanagenzi imetimiza miaka mitano tangu kuanzishwa kwake, na imeendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuwaandaa wanafunzi kupitia uzoefu wa moja kwa moja kazini, kuimarisha ujuzi wa kiutendaji, na kupanua mtandao wao wa kitaaluma kama sehemu ya maandalizi ya kuingia kwenye soko la ajira.