ISW yaingia makubaliano na One Tanzanite Football Academy kuboresha viwanja vya michezo
12 November 2025
Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) kimeingia makubaliano na One Tanzanite Football Academy ya kuboresha Viwanja vya michezo #ISW Makubaliano hayo yameingiwa leo tarehe 11 Novemba, 2025 kati ya Dkt. Joyce Nyoni, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii pamoja na Bw. Agapiti Emmanuel, Mkurugenzi Mtendaji wa One Tanzanite Football Academy. Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Timu ya Menejimenti ya #chuochaustawiwajamii na Baadhi ya maafisa kutoka One Tanzanite Football Academy.