Mhadhara wa kuwajengea wanafunzi uelewa masuala ya uhamiaji wafanyika ISW
03 September 2026
TAASISI ya Ustawi wa Jamii (ISW), kupitia Idara ya Taaluma za Kazi kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO), imefanya mhadhara wa umma uliolenga kuwajengea uelewa wanafunzi kuhusu changamoto za uhamiaji wa nguvu kazi na ushiriki wa vijana katika uhamiaji salama. Mhadhara huo wa kitaaluma uliofanyika Juni 12, 2026 ISW kampasi ya Dar es Salaam, uliongozwa na kaulimbiu ya "Tanzania Labour Migration Framework and Youth Engagement in Safe Migration." (Mfumo wa Tanzania wa Uhamaji wa Wafanyakazi na Ushiriki wa Vijana katika Uhamaji Salama wa Kikazi). Lengo kuu la mhadhara huo lilikuwa ni kutoa uelewa mpana kwa wanafunzi juu ya changamoto mbalimbali zinazohusiana na uhamiaji wa wafanyakazi na kuwaelewesha sababu zinazowafanya watu wengi kukimbilia nje ya nchi kutafuta ajira. Aidha, mkusanyiko huo ulikusudia kuwahamasisha na kuwandaa wanafunzi kushiriki kikamilifu katika kampeni za uhamiaji salama (safe migration) pamoja na kuwa mabalozi wa kutoa elimu na taarifa sahihi kwa jamii inayowazunguka ili kuepuka majanga kama usafirishaji haramu wa binadamu. Na Mwandishi wetu 2 Mhadhara huo ulitawaliwa na mijadala ya kina iliyowezeshwa na wataalamu wabobezi kutoka ILO-Tanzania, wakiongozwa na Mshauri Mkuu wa Kiufundi, Aida Awel, Mratibu wa Kitaifa wa Mradi, Diana Rutrchura), pamoja na Ofisa Mawasiliano wa Kitaifa/National Communication Officer, Yonas Zewdie. Wataalamu hao walichambua kwa kina mifumo ya kisheria na kisera inayolinda haki za wafanyakazi wanaohama, na namna vijana wanavyoweza kutumia fursa za kikanda kwa njia salama na halali. “Tukio hili lilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, kwani limewapa fursa ya nadharia kukutana na vitendo kwa kujifunza moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa mashirika ya kimataifa,”amesema Mkuu wa Idara ya Taaluma za Kazi na Menejimenti ya Umma, Dkt. Jumanne