Government Emblem

The United Republic of Tanzania

Chuo cha Ustawi wa Jamii

Institute Logo

Kongamano la Kimataifa la Uwezeshaji Watu, Ustawi Lafikia Malengo

03 September 2026
Kongamano la Kimataifa la Uwezeshaji Watu, Ustawi Lafikia Malengo
Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) kimekamilisha kwa mafanikio Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Uwezeshaji wa Watu na Ustawi. Tukio hilo la kihistoria lilifanyika tarehe 5 Juni 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). Likiongozwa na kauli mbiu "Kuwezesha Watu na Kubadilisha Jamii: Njia za Ustawi Endelevu," kongamano hilo lilifunguliwa rasmi na Mgeni Rasmi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima. Mkutano huo ulijumuisha uwasilishaji wa mada na mijadala kutoka kwa wasomi, watafiti, watunga sera, na wadau wa maendeleo kutoka zaidi ya nchi 11 duniani. Akizungumza kuhusu kongamano hilo, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Dkt. Joyce Nyoni amesema ushiriki huu mpana wa kimataifa ulileta pamoja wataalamu mashuhuri, wakiwemo wasomi kutoka mataifa kama Hungary, Uganda, Norway, Nigeria, na Namibia. Na Mwandishi wetu 5 Aidha, amesema suluhisho na mikakati iliyojadiliwa inatarajiwa kusaidia watunga sera kuunda mbinu bora za kulinda makundi yaliyo katika mazingira magumu, kupunguza umaskini, na kuinua viwango vya maisha vya wananchi. Dkt. Joyce amesema kongamano hilo limeacha alama muhimu katika sekta ya ustawi wa jamii nchini na kimataifa, likithibitisha kuwa uwezeshaji wa wananchi ndio msingi wa mabadiliko endelevu. Maazimio yaliyofikiwa wakati wa kufunga tukio hili yanatarajiwa kufanyiwa kazi na wadau mbalimbali, ili kubadili nadharia zilizojadiliwa kuwa vitendo vyenye tija kwa maendeleo ya taifa.
Institute Logo