Government Emblem

The United Republic of Tanzania

Chuo cha Ustawi wa Jamii

Institute Logo

Watumishi bora 2025 na wa muda mrefu wapongozwa - ISW

19 August 2026
Watumishi bora 2025 na wa muda mrefu wapongozwa - ISW
Menejimenti ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, leo tarehe 15 Mei, 2026 imewatambua watumishi walioibuka watumishi bora kwa mwaka 2025, pamoja na wale ambao wameitumikia taasisi kwa zaidi ya miaka mitano, kwa kuwapa vyeti na mkono wa pongezi. Akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Taasisi, Dkt. Joyce Nyoni, amewapongeza watumishi walioibuka bora zaidi katika mwaka 2025. "Kutambua wafanyakazi hodari ni moja ya motisha ya kuleta chachu ya kufanya kazi kwa bidii zaidi, lakini pia ni sehemu ya wengine kuiga mfano ili kupokezana kijiti hiki cha kuwa mfanyakazi bora," amesema Dkt. Joyce. Kwa watumishi wote, naomba niwapongeze sana na kuwashukuru kwa kuwa sehemu ya mafanikio ya taasisi yetu, na niwaombe muendelee kuchapa kazi." Aidha, watumishi wa ISW katika hafla hiyo walipata mafunzo kutoka kwa wataalam kutoka WCF na OSHA kuhusu masuala ya usalama mahala pa kazi, mbinu za kuhakikisha wanakuwa salama katika maeneo ya kazi, pamoja na mafao ya wafanyakazi pale wanapopata ajali au kuumia kazini.
Institute Logo