Government Emblem

The United Republic of Tanzania

Chuo cha Ustawi wa Jamii

Institute Logo

Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi ISW

19 August 2026
Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi ISW
Afisa Kazi Mwandamizi Neema Daniel Msyaliha kutoka Idara ya kazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano tarehe 23 Machi, 2026 kwa niaba ya Kamishna wa kazi, amezindua Baraza jipya la Wafanyakazi la Taasisi ya Ustawi wa Jamii ambalo litahudumu kwa miaka Mitatu. Katika kikao hicho, Baraza la Wafanyakazi lilipokea na liliwatambua na kuwathibitisha wajumbe wapya kutoka katika idara na vitengo mbali mbali. Katika Hatua nyingine Baraza lilifanya uchaguzi wa katibu na Katibu msaidizi wa baraza hilo jipya na baadaye kujadili masuala mbali mbali ya maendeleo ya Taasisi ikiwepo Dira ya mpango mkakati wa Taasisi pamoja na Kupitia Rasimu ya Bajeti ya Taasisi ya Mwaka 2026/2027.
Institute Logo