Wanawake ISW wawagusa kwa zawadi wagonjwa Zahanati ya Kijitonyama
09 March 2026
Kuelekea kilele cha Siku ya Mwanamke Duniani, Wanawake wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, tarehe 6 Machi 2026, wakiongozwa na Naibu Mkuu wa Chuo Utawala Dkt. Zena Mabeyo wametembelea na kutoa zawadi mbalimbali Zahanati ya Kijitonyama zitakazosaidia kuboresha huduma katika Wodi ya Wazazi. Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Dkt. Faraja Mgana amesema ni heshima na upendo mkubwa ambao wanawake wa ISW wameonyesha kwa wagonjwa wanaopata matibabu kwenye zahanati hiyo, lakini zaidi tendo hili limedumisha mahusiano mazuri na ujirani mwema kati ya Chuo cha Ustawi wa Jamii na Zahanati ya Kijitonyama.