Chuo cha Ustawi wa Jamii

ISW YAINGIA MAKUBALIANO NA ONE TANZANITE FOOTBALL ACADEMY KUBORESHA VIWANJA VYA MICHEZO

Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) kimeingia makubaliano na One Tanzanite Football Academy ya kuboresha Viwanja vya michezo #ISW Makubaliano hayo yameingiwa leo tarehe 11 Novemba, 2025 kati ya Dkt. Joyce Nyoni, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii pamoja na Bw. Agapiti Emmanuel, Mkurugenzi Mtendaji wa One Tanzanite Football Academy. Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Timu ya Menejimenti ya #chuochaustawiwajamii na Baadhi ya maafisa kutoka One Tanzanite Football Academy.

MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI YAKABIDHI JUZUU ZA MAAMUZI YA MIGOGORO YA KAZI KWA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi, Dkt. Y. J. Mlyambina, tarehe 10 Oktoba 2025, amekabidhi Juzuu za Maamuzi ya Migogoro ya Kazi kwa Chuo cha Ustawi wa Jamii. Dkt. Mlyambina alikabidhi nakala mbili (2) za Juzuu za Maamuzi ya Migogoro ya Kazi Mahakama Kuu ya Tanzania pamoja na nakala sabini (70) za Labour Court Case Digest, akiwa ameambatana na mahakimu wa Mahakama Kuu. Juzuu hizo zimepokelewa na Naibu Mkuu wa Chuo – Fedha na Utawala, Dkt. Eventus Mugyabuso, kwa niaba ya Mkuu wa Chuo. Juzuu za Maamuzi ya Migogoro ya Kazi zinahusu kesi zilizotolewa maamuzi kuanzia mwaka 2010 hadi 2024, na zinatarajiwa kusaidia wanafunzi, wanazuoni wa sheria na watafiti kupata rejea sahihi na kuelewa mwenendo wa tafsiri za kisheria katika migogoro ya ajira nchini. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Jaji Mlyambina amesema kuwa kuleta Juzuu hizo Chuo cha Ustawi wa Jamii ni heshima ya Kutambua mchango na kazi inayofanywa na chuo cha Ustawi wa Jamii, ambacho ni chuo pekee nchini kinachotoa taaluma za kazi na kuzalisha maafisa wanaokwenda kufanya kazi katika Mahakama za Kazi kama wasuluhishi na watatuzi wa migogoro ya ajira. Kwa Upande wake Naibu Mkuu wa Chuo #ISW Dkt. Eventus Mugyabuso amemshukuru sana Jaji Mlyambina kwa Kuona umuhimu wa kuleta Juzuu hizo #ISW ambazo zitaongeza ujuzi kwa wanafunzi wa Taaluma za kazi na wanazuoni kwa ujumla.

MAADHIMISHO YA WIKI YA USTAWI WA JAMII

Watumishi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii washiriki Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Ustawi wa Jamii yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ustawi wa jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam Agosti 30, 2025. Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Dkt. Philip Isdor Mpango akiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum - Dkt. John Jingu. Aidha Mgeni rasmi alizindua Kampeni ya "PATA MSAADA WA KISAIKOLOJIA; IMARISHA AFYA YA AKILI" , Sera ya Taifa ya Wazee 2003 (Toleo la Mwaka 2024), Kitini cha Wawezeshaji wa Mafunzo ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto na Kitini cha Ufundishaji wa Watoa Huduma za Afya ya Akili, Msaada wa Kisaikolojia na Kijamii kwa Vijana Balehe.

WAZIRI WA MJJWMM MHE. DKT. DOROTHY GWAJIMA ATEMBELEA BANDA LA ISW KWENYE MAONESHO YA WIKI YA USTAWI WA JAMII

Mratibu wa kituo cha Elimu, Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia, Rufina Khumbe akitoa maelezo kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima alipotembelea banda la ISW katika Maonesho ya Wiki ya Ustawi wa Jamii 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii.

KITUO CHA ELIMU, USHAURI NA MSAADA WA KISAIKOLOJIA KIMEWATEMBELEA WANAFUNZI WA KILUVYA SEKONDARI

Kuelekea Wiki ya Ustawi wa Jamii, Kituo cha Elimu, Ushauri na Msaada wa Kisaikolojia kilitembelea Shule ya Sekondari Kiluvya tarehe 9 Agosti 2025 na kuzungumza na wanafunzi wa Kidato cha Tano kuhusu mada za ukatili wa kijinsia, mahusiano na mawasiliano, pamoja na Career Guidance. Mada hizi ziliwasilishwa kwa mbinu shirikishi na zenye kuhamasisha ushiriki wa wanafunzi.

MKUU WA CHUO DKT. JOYCE NYONI ATEMBELEA BANDA LA ISW, MAONESHO YA NANENANE

Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni, ametembelea banda la #ChuoChaUstawiWaJamii katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma, tarehe 8 Agosti 2025. Dkt. Nyoni alipokea maelezo kutoka kwa Mhadhiri Msaidizi Abubakar Fadhili na Mhadhiri Msaidizi Salama Limei kuhusu kozi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, pamoja na huduma za elimu na msaada wa kisaikolojia zinazotolewa kwa wananchi wanaotembelea banda hilo.

KOZI YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO

Kwa mwaka huu wa masomo 25/26 Chuo cha Ustawi wa Jamii kinadahili kozi muhimu na yenye fursa nyingi za Kujiajiri na kuajiriwa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa ngazi ya Certificate na Diploma ambayo inatolewa katika kampasi ya Kisangara, Mwanga pekee. Kozi hii itaandaa wataalam ambao watahakikisha mtoto anakuwa katika utimilifu wake; kiakili, kimwili, kijamii, kihisia, lugha, kiimani na kimaadili. Ili mtoto aweze kufikia utimilifu wake ni lazima apate afua mbalimbali ikiwa ni pamoja na afya, lishe bora, malezi yenye mwitikio, afua za ufunzaji wa awali, ulinzi na usalama, na uchangamshi wa awali. Wahitimu wa Kozi hii wanaweza kujiajiri lakini pia kuajiriwa katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kwenye vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya afya, katika dawati la mama na mtoto, makao ya watoto, kwenye madawati ya watoto, mashuleni, na kwenye mashirika yasio ya kiserikali ya kitaifa na kimataifa. Tunawakaribisha sana Wahitimu wa kidato cha nne na sita na wote ambao wangependa Kupata ujuzi adhimu wa kozi hii kufanya maombi ya Kozi hii pindi dirisha la awamu ya pili ya Udahili wa Certificate na Diploma utakapo funguliwa.

ZIARA YA KITAALUMA

Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii watembelea kiwanda cha Kiboko Continuous Galvanizing Line kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam. Lengo la ziara hii lilikuwa kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu afya na usalama mahala pa kazi na kuona kwa karibu uhalisia wa yale wanayojifunza darasani.

Maonesho ya Sita ya Elimu ya Juu Zanzibar

Chuo cha Ustawi wa Jamii kilishiriki Maonesho ya Sita ya Elimu ya Juu Zanzibar, 14 Julai - 20 Julai 2025. Ilikuwa ni wakati mzuri wa Chuo kukutana na wanafunzi wa kidato cha sita wenye ndoto kubwa ya kujiendeleza kitaaluma.

TEXAS UNIVERSITY WATEMBELEA ISW

Wahadhiri na wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Texas, Marekani watembelea Chuo cha Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kitaaluma na kutambua fursa za ushirikiano katika nyanja za utafiti, ubadilishanaji wa maarifa na maendeleo ya kitaaluma. Ziara hii ni hatua muhimu kuelekea kujenga ushirikiano wa kimataifa unaolenga kuinua ubora wa elimu inayotolewa taasisi.

Kumbi za Mihadhara Kuongezwa ISW

Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dkt. Joyce Nyoni, amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa mapya unaoendelea katika Kampasi ya Dar es Salaam, ambapo hadi sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 16 na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo Mwanzoni mwa Mwaka 2025. Mradi huu unalenga kuboresha miundombinu ya kujifunzia katika kampasi ya Dar es Salaam.

Announcements
Joining Instructions 2025-08-21 15:22:20
SELECTED CANDIDATES FOR ADMISSION INTO CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES (KIJITONYAMA AND KISANGARA CAMPUSES) 2025-2026 ACADEMIC YEAR ( SECOND ROUND) 2025-11-12 06:59:51
First Semester Class Timetable - DSM Campus 2025-11-11 05:41:10
ORIENTATION AND REGISTRATION TIMETABLE 2025-2026 2025-11-10 12:13:02
Supplementary and Special Examination Timetable. Bachelor Degree - Kisangara Campus 2025-11-10 11:43:46
SUPPLEMENTARY AND SPECIAL EXAMINATION TIME TABLE FROM 17 TO 19 NOVEMBER 2025 2025-11-10 09:24:06
SECOND SEMESTER SUPPLIMENTARY & SPECIAL EXAMINATION TIMETABLE NOVEMBER 2025 REVIEWED 2025-10-27 13:31:57
SELECTED CANDIDATES FOR ADMISSION INTO BACHELOR DEGREE PROGRAMMES (KIJITONYAMA AND KISANGARA CAMPUSES) FOR THE 2025/2026 ACADEMIC YEAR (Round 1-3) 2025-10-20 06:18:47
Selected Students for Hostel Accommodation 2025/2026 (Batch 1) 2025-10-17 12:53:37
HATUA ZA KUTENGENEZA CONTROL NUMBER ZA MALIPO YA ADA 2025-10-16 07:19:36
SECOND SEMESTER SUPPLEMENTARY EXAMS TIMETABLE FOR BACHELOR DEGREE KISANGARA CAMPUS NOVEMBER 2025 2025-10-09 05:53:09
CALL FOR APPLICATION FOR VARIOUS ACADEMIC PROGRAMMES-ACADEMIC YEAR 2025-2026 (THIRD ROUND) 2025-10-03 12:06:06
CALL FOR PROPOSAL 2025-2026 2025-09-15 05:19:47
CALL FOR JOURNAL ARTICLES 2025-2026 2025-09-15 05:19:25
SUPPLEMENTARY & SPECIAL EXAMS TIMETABLE FOR NTA 4 & 5. SEM II - 2024-2025. - Kisangara campus 2025-08-25 13:04:56
SUPPLEMENTARY & SPECIAL EXAMS TIMETABLE FOR NTA 4 & 5. SEM II - 2024-2025. - Kisangara campus 2025-08-25 07:09:20
TANGAZO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA TAMISEMI 2025-08-18 14:42:21
SELECTED CANDIDATES FOR ADMISSION INTO BASIC TECHNICIAN CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMMES ROUND 1 2025-08-14 14:47:37
JARIDA LA MTANDAONI APRILI - JUNI 2025-08-07 12:26:34
STUDENT'S ACCOMMODATION APPLICATION FORM 2025-07-02 12:31:54
ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA OFISI YA RAIS-TAMISEMI KUJIUNGA NA CHUO CHA USTAWI WA JAMII - 2025-2026 2025-06-17 07:34:57
TANGAZO - WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA TAMISEMI MWAKA WA MASOMO 2025-2026 2025-06-11 12:42:14
Jarida la Mtandaoni Januari - Machi 2025 2025-04-30 07:35:13
Jarida la Mtandaoni Oktoba - Desemba 2025-01-22 05:10:45
Jarida la Mtandaoni July - September 2024 2024-10-31 12:48:49
FEE STRUCTURE 2025/2026 ACADEMIC YEAR 2024-08-26 10:11:55
Site Visitors
Today
449
Yesterday
2,025
This Week
14,577
This Month
53,575
All days
866,960
Online
5
Video